Hapa kuna wahitimu wawili; wa Kwanza alihitimu miaka 10 iliyopita, anahangaika duniani ni kama Kaini wa Biblia aliyemuua nduguye Abeli, ingawa adhabu ya huyu muhitimu imechangiwa na ufisadi kutokana na mpangilio potovu wa ajira. Haya, Kuna wa pili ambaye alihitimu mwaka mmoja uliopita na tayari ameingizwa katika huduma ya Umma, cheti chake sawa na wa kwanza!

Je, tofauti kati yao itakuwa nini? Sio bidii ya Wapili, ni kwasababu anajuana na ‘Bwana Kubwa’ mle ndani. Huyu ndiye alimshika  mkono akampitisha mlango wa nyuma. Halafu kuna kundi kingine ambao wanaweza hongana  KES. 300,000 au zaidi ili kupata nafasi hizi. Lakini wa kwanza ameshindia mahangaiko kwa Jua kali, amejaribu kubisha makampuni, idara tofauti na hafanikiwi.  Hana mwingine wa kumkimbilia ila Mola., ameshindia kufunga na kuomba hata koo imekauka, magoti yamechujuka juu ya dua zake, sasa muongo moja umeisha na bado hajabahatika.

Hili swala la Usawa katika Ajira ya Umma lazima lishughulikiwe sasa, itabidi serikali ichukue, hatua Tatu ili kurejesha Usawa;

La Kwanza: Pawe na Shirika Kuu la Uajiri kwa Watumishi wote wa Umma, ili idara yoyote inayohitaji wafanyakazi iweze kupeleka tangazo la nafasi na vyeti hitajika  kwa shirika hilo la uajiri.

La Pili: Katika kaunti zote 47, pawe na Idara ya Usajili ya wahitimu kulingana na mwaka wa kuhitimu na pia kiwango cha Masomo. Kisha tufuate mpangilio wa uteuzi kutoka Kaunti zote. Wale walihitimu kwanza wapewe kipao mbele sababu wamechomeka na jua sana. Si haki mwenye alimaliza hivi majuzi anavukishwa laini.

La Tatu: Idadi ya waajiriwa iwe na Sura ya Kitaifa, isikue tu ni jamii za Rais na Naibu wake pekee ndio wananyakua vinono ilhali jamii zingine wameshindia skuma wiki. Pia kuna Jamii kutoka mikoa ya Ugumu Fulani kutokana na athari za mazingira yao, pia wapewe kipao mbele, wafikiwe pia. kwa kifupi tunataka haki itendeke kwa wakenya wote.

Idara ya KRA hivi majuzi ilijipata pabaya mahakamani kwa kutozinngatia Usawa kwenye nafasi za Ajira, jaji ya mahakama ya Ajira aliwakosoa kamati ya ajira kwa kupeana nafasi 80% kwa jamii mbili tu, na nikutoka Jamii ya Rais na naibu wake. Na hii ndio shida babu mkubwa hapa Kenya, Ukabila watumiliza.

Idara za Jeshi na Polisi wanafuta mfumo huu, vile vile Tume ya Huduma za Walimu TSC inafuata mfumo huo huo, mbona hatufuati huo mfumo pia katika ajira zote za umma? Mbona tumewachia wachache wafaidi jamaa zao na kuziuza kwa milango ya nyuma?

Miongo iliyopita serikali ilifuata mfumo huo, lakini kwa utepetevu wao tumejikuta Shakahola. Uajiri kwa Huduma za Umma ulikuwa ukifanyika kwenye Makao Makuu ya Wilaya, itabidi turudi hapo. Hii kasumba ya ‘Bwana kubwa’ au ‘Dongera fulani’ ni SUMU BARIDI kwa taifa letu, inatumaliza.Itakuaje Jamii Fulani wameshinda Kula Nyama ilhali wengine wameshinda kumezea tu Mate, hatutakubali kamwe, Kenya ni yetu sisi wote!

Huyu swara tunamwinda sisi sote, sasa itabidi turejeshe usawa kwenye ugavi, angalau hata Matumbo yafikie wengine aise! Wengine tumechoshwa kumeza mate tu!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)