Mheshimiwa Rais, uliposhika hatamu ya uongozi uliinua matumaini kwa wanyonge maarufu kama ‘Mama Mboga na Watu wa Boda Boda’. Kwa ahadi yako, wengi walijitokeza wakaanzisha biashara wakitarajia serikali yako ingewawezesha kusonga mbele, wengi walitarajia uzinduzi wa njia mkopo ili waweze kuinia biashara zao kama ulivyowaahidi. Lakini kwa sababu zisizoeleweka ahadi yako ililoa kwa mafuriko tuliyoshuudia hivi majuzi. Hata hivyo baadhi ya mahasla wameendelea kujikaza, lakini la kusikitisha ni kwamba maafisa wa utekelezaji kenye idara tofauti za serikali wanadhulumu mahasla sana. Hawa maafisa wa utekelezaji wameshindia kupora mihela kwenye biashara za vijana, wengi wanalia na wengine hata wamekatizwa hiyo tamaa ya kuchapa kazi.
Mara tu hasla ameanzisha kabiashara Askari wa Serikali ya Kaunti maarufu kama ‘Kanjo’ washamvaamia. Wanamkamata na kama ilivyo desturi watamuachilia baada ya kupokea hongo. Mnyonge anaamua badala ashindie kuvaamiwa na Kanjo ni heri ajikaze alipe ada yao atulie, maskini alidhania huo ndio mwisho wa uvamizi, kumbe kutulia ni kifungulia mlango manyang’au wengine wanyakue.
Muda mfupi baadaye, maafisa wa Kenya Power (KPLC) wamefika! Ati jamaa amevuta umeme bila kufuata taratibu zinazofaa! Lakini kwa kweli, haka kabiashara hakawezi lipia Mita ya KPLC. Alichokifanya ni kwamba alieka sabmita na akakubaliana kuliipia matumizi yake, lakini bill yote ya Main italipwa tu, maafisaa wa Kenya Power hawataliiskiza hilo. Basi wao pia wanawavamia mahasla ati kupeleka korokoroni, watadai zikiwa kidogo KES. 10,000 ndio wamuachilie maskini hasla, na ndio waendelee kutumia umeme huo watakua wakiwalipa Maafisa kakitu kila wakati.
Wanaofuatilia sasa ni maafisa wa KRA, wanadai ajisajilishe na mfumo wa eTIMS, na katika hiyo ziara ya kidharura wameitisha vitabu vya hesabu za fedha za miaka mitatu iliyopita! Jamani Kibanda itauza sigara ya sh.5 au dawa mende ya sh. 10 na eTIMS? Printer ya eTIMS yadai umeme na Kenya Power walishampokonya umeme. Sheria ya VAT yasema wazi biashara zinazo uza takribani Millioni 5 kwa mwaka ndio yafaa wauze na VAT, sasa jamani haka kakibanda hakaezi fikisha hata 10,000 kwa mwezi! Mafisa wa KRA wamekua kero sana kwa mahasla, basi wao pia utakuta amekuekea kwa system zao ada zisizo eleweka kidogo kidogo ndio hao wanakudai, umuone kando ‘akupunguzie’.
Mnyonge akinunua Subwoofer asikilize muziki akipitisha masaa mle kibandani, hapo sasa amevutia mafisi kutoka Music Copyright Society of Kenya (M.C.S.K). Wanamvamia kwa madai ya kucheza muziki bila leseni. Bila shaka kuachiliwa ni ‘Ucheze kama Wewe’ ndio wakuachilie.
Ikiwa mnyonge anashughulika na bidhaa kama za urembo, huyo sasa amejieka kwa mtego wa halmashauri ya Kupambana na bidhaa bandia yaani Anti-Counterfeit Authority (ACA)! Utaskia ACA wamepanga ‘msako’ wa bidhaa bandia, kumbe wamelenga viosk na maduka ya mahasla, hatujashuhudia ACA wakivamia biashara ya mabwenyeye, mie sina shida yeyote na utekelezaji wa sheria, lakni itakuaje ‘utekelezaji’ ni kulenga tu vya wanyonge?
Kawaida bidhaa hizi huagizwa kutoke inje ya nchi, bidhaa bandia hupitia bandarani wanako maafisa wa utekelezaji, halafu bidhaa husafirishwa hadi Nairobi na kuekezwa kwa godown, swala ni ACA wako wapi kenye huu mkondo wote? Mbona wangoje ‘bidhaa bandia’ zifikie mnyonge ndio waanzishe msako? Maskini anavaamiwa na kupokonywa bidhaa zake, kuachiliwa ni KES. 10,000. Halafu jamani, counterfeit ni nini? Leo akiamka aamue unachokiuza ni ‘Counterfeit’ Ole wako utajikojolea surualini!
Ujikute kwenye biashara ya Kuuza Bateri za gari, shida tupu! Huyu sasa anavutia Anti-Radiation. Tuhuma ya kwanza ni kwamba betri hizo zinatoa mawimbi ya redio na hazijaidhinishwa. Wazi wazi Betri ni ya Exide Chloride, kamwe hawataenda makao makuu ya Kampuni Chloride kuidhinisha madai, hiyo ya duka ya mnyonge tu ndio inawavutia. Mafisi wanamvamia kuachiliwa ni hongo takriban KES. 10,000.
Ole wake ikiwa ikiwa anauza vileo, yaani Wines na Spirits, huyu sasa amezingirwa na mamba! Haijalishi ako na lesseni zote na anauza pombe halali, hapa lazima uingie kwenye ‘Mukataba’ na OCS (Kamanda wa Polisi) wa eneo lako utoe ada ya ulinzi, la sivyo atashindia kukukamata na kukupeleka Kotini kwa madai gushi. Mambo hapa ni matatu, usalimu amri yake, Ushindie kumtolea ada ya Ulinzi au ufunge biashara yako.
Ikiwa biashara ni kuuza vitu kama unga unga hivi, wewe kaa ukingoja Anti-Doping Agency! Shirika la Kupambana na madawa ya Kulevya ndio sasa wanakuotea, watakushuku kwa kuuza madawa au kueka chembe chembe za madawa kwenye bidhaa zako. Hawa pia watadai kubeba sampuli waipeleke kwenye mahabara kuichunguza kama kunako chembe chembe za madawa. Utakua ushavamiwa na stock yako pia imeenda. Hapa gharama ya kuachiliwa iko juu kiasi.
Kwa wale wanauza Uji Power na kahawa, vibandani au sokoni mtakuwa katika mchezo wa paka na panya na maafisa wa afya wa Kanjo, Ukubali kutoa ada ya ulinzi ndio uendelee ama pia wakufungie ajira yako.
Serikali ya wanyonge ambayo iliingia na matumaini mengi kwa wanyonge sasa imekuwa ‘La Torementa’ yaani Mtesi wa Mama Mboga na Watu wa Boda Boda. Maafisa wa Utelezaji wamegeuka ‘Mafisi wa Serikali’,jamani nauliza tu, haka kabinda mumeshinda kukikavamia hivi katabaki kweli? Ubuntu wenu uko wap? Nyakua Nyakua kila uchao si ataisha, si mumemrudisha nyumbani pale jobless Kona. Ndio huyo hawezi jikimu kimaisha, amelemewa hata kumlea mtoto wake, maandamano ikiitishwa nani watajitokeza? Si ni hawa manyang’au wako walipora wakaisha.
Kupata ajira nchini Kenya ni kama kuvuka mto mamba! Labda uwe na ‘Uncle Bigi’ akuingize kwa mlango wa nyuma au uko uwezo wa kutoa Ksh. 300,000 hongo ndio wakuajiri. Hata hivyo kuna wale ambao wamejitokeza kuanzisha biashara angalau watjitafutie sabuni, serikali yapaswa kuwachunga dhidi ya Mafisi wafisadi. Serikali bora yafaa iwatafutie namna ya kupata mikopo wasonge mbele. Lakini hii yako ni nyakua nyakua kila uchao, watanawiri aje?
Hivyo basi Mhe. Rais unapaswa kutoa ilani kali kwa hawa mafisi wako, wakanye wamepora mahasla ya kutosha sasa. Kadhalika yafaa uzindue utaratibu wa Kusajilisha biashara za mahasla kwa Kila Kaunti ndio mafisi wapitie kando na hizo Vioski. Hawa Mafisi ni SUMU BARIDI, watakuharibia uongozi wako!
Hata dadangu tulimwanzilisha biashare apate angalau kaunga, tukashindia kumnusura kwenya mafisi wako, mwishowe tulichoka, alipolemewa na hawa mafisi wako aliifunga hiyo biashara, nikimwona anashiriki maandamona sitamkashifu, naelewa ni ghadhabu aliyo nayo!